UONGOZI SINGIDA WATOA TAMKO KUHUSIANA NA MANYIKA KUJIWEKA KANDO
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Singida United kupitia kwa Mkurugenzi wake, Festo Sanga, umesema kuwa hkuna madai ya fedha baina yake na kipa Manyika Peter ambaye ameshajiweka kando kuichezea timu hiyo.
Sanga ameeleza mpaka sasa Manyika ameshaitumikia Singida kwa muda wa mwaka mmoja na amebakiwa na mmoja mwingine huku akisema stahiki zake na malipo ni siri baina ya klabu na mchezaji.
Mkurugenzi huyo amesema si kila kitu kinapaswa kuwekwa hadharani na badala yake inawekwa kama siri ingawa amekazia kuwa Manyika bado ni sehemu ya Singida United.
Kipa huyo aliyesajiliwa akiwa huru baada ya msimu wa 2016/17 kumalizika, ameamua kuvunja mkataba wake kutokana na kutolipwa baadhi ya stahiki zake ambazo walikubaliana kwenye mkataba na Singida ikiwemo fedha za usajili.
Klabu hiyo iliyokuja kwa kasi imeanza kuwa katika ripoti hasi juu ya ulipaji mishahara wa wachezaji huku haijajulikana tatizo limetokea wapi ukiangalia ina udhamini na makampuni kadhaa ya kibiashara.








0 COMMENTS:
Post a Comment