SANE, ZAHA, BECKAM, SHAW: HABARI KUBWA NA MUHIMU LEO ALHAMIS
Leroy Sane atalazimika kuimarisha tabia yake kwa yeye kuweza kufanikiwa kulingana na mchezaji mwenza wa Ujerumani Toni Kroos.
Kwa mujibu wa BBC, Sane mwenye umri wa miaka 22 aliwachwa nje ya kikosi cha Ujerumani cha kombe la dunia lakini amerudi kwa mechi ya Uefa dhidi ya Ufaransa mbali na mechi ya kirafiki ya siku ya Jumapili dhidi ya Peru.
Lakini bado hajaanzishwa katika klabu yake ya City msimu huu na aliwachwa nje siku ya Jumamosi.
Mara nyengine unapata anavyohisi kutokana na tabia yake na ni muhimu sana iwapo tunashinda au kupoteza.
''Ni mchezaji ambaye ana kila kitu unachohitaji kuwa mchezaji bora, lakini mara nyengine lazima umwambie kwamba ni sharti aonyeshe kiwango cha juu cha mchezo'', aliongeza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Real Madrid.
Sane alishinda taji la mchezaji chipukizi la 2017-18 baada ya kufunga magoli 10 na kutoa usaidizi wa mabao 15 katika ligi ya Uingereza msimu uliopita.








0 COMMENTS:
Post a Comment