Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, ameibuka na kueleza kuwa hakuna kiongozi Simba ambaye atakaa ndani ya madaraka milele.
Manara amesema kuwa viongozi wote waliopo wapo kwa dhamana na hakuna atayeendelea kuwa mtawala siku zote za maisha yake kwa kuwa kuna muda maalum.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya Manara kukasirishwa na tukio la kurushiwa chupa za maji baada ya mechi na Mbao ambayo Simba ililala kwa bao 1-0.
Vilevile Manara amewataka mashabiki wa Simba kuacha tabia hizo ambazo hazina mashiko ya msingi kwani hakuna kiongozi anafurahia kufanyiwa vurugu hivyo wote waliopo wataondoka.
Manara bado ameonekana kusikitishwa zaidi na tukio hilo huku akifunguka kuwa kuna wakati anaona vema akaachana na masuala ya soka lakini hawezi kuisaliti kazi yake kwa maana bado anategemewa.








Viongozi mnanishangaza mnaposhindwa kwa na uvumilivu wa kasha za kuongoza vilabu vikubwa kama vya Simba na Yanga. Unazungumzia klabu yenye wanachama na wapenzi mashabiki takriban asilimia 45 ya watanzania kwa kila timu ya Simba na Yanga. Anapotokea mtu mmoja shabiki au watatu wakarusha chupa uwanjani. Hilo sio uamuzi wa mashabiki lote asilimia 45. Hilo ni tukio la mvunja amani mmoja au watatu, askari wawakamate has na kuwachukulia hate ipasavyo. Mashariki kweli want malalamiko yao wana uchungu fulani,viongozi hamtaki kusikia, lakini yapo malalamiko, lakini hayo hayatoi ruhusa ya kurusha chupa za maji, habana. Lazima njia za kistaarabu zitumike. Lakini viongozi lazima muelewe nyinyi sio miungu wala sio malaika, wapo mnaowakosea na sapo wanaowakosea. Mkubali dhamana ya uongozi. Kwangu mimi dclili ya mtu mmoja kutupa chupa ya maji ni jambo la kutoka kujitafakari na kuchukua atua ya kuona wapi kuna kero na mapungufu, ya kujirekebisha.
ReplyDeleteViongozi mnanishangaza mnaposhindwa kuwa na uvumilivu wa kadhia za kuongoza vilabu vikubwa kama Simba na Yanga. Unazungumzia klabu yenye wanachama na wapenzi mashabiki takriban asilimia 45 ya watanzania wote kwa kila timu ya Simba na Yanga. Anapotokea mtu mmoja shabiki au watatu wakarusha chupa uwanjani, hilo sio tukio au uamuzi wa mashabiki wote asilimia 45. Hilo ni tukio la mvunja amani mmoja au watatu, kwanini askari wasimkamate hapohapo na kuwachukulia hatua ipasavyo?. Mashabiki kweli wana malalamiko yao na wana uchungu fulani,viongozi hamtaki kusikia, lakini yapo malalamiko, lakini hayo hayatoi uhalali wa tabia mbovu ya kurusha chupa za maji, hapana. Lazima njia za kistaarabu zitumike. Lakini viongozi lazima muelewe nyinyi sio miungu wala sio malaika, wapo mnaowakosea na wapo wanaowakosea. Mkubali dhamana ya uongozi. Kwangu mimi kitendo cha mtu mmoja kutupa chupa ya maji ni jambo la kujitafakari na kuchukua hatua ya kuona wapi kuna kero na mapungufu ya kujirekebisha. Kwakuwa wapenzi wa timu yenu hawakupaswa kutenda kosa hilo, ni wazi kuna jambo linawakera. Vizuri kujenga mazingira ya kuwepo kwa amani ndani ya klabu kwa kwa sensitive na hate zinazochukuliwa na viongozi ambazo zinaweza kuathiri hisia za mashabiki wa timu yao. Kiongozi engine hata ushauri tu hawataki kusikia sasa jiulize huyo sio anakaribisha vurugu kwenye klabu?
ReplyDelete