September 17, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema kukosekana kwa Kocha wake Msaidizi, Mrundi Masoud Djuma, si sababu ya timu hiyo kwenda suluhu na Ndanda FC.

Simba ilikuwa na kibarua cha mchezo wa Ligi Kuu Bara Jumamosi ya wiki jana kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona ambao ulimalizika kwa suluhu tasa ya 0-0.

Manara amesema kukosekana kwa Djuma hakujabadilisha chochote na hata kama angekuwa matokeo ya aina yoyote ile yangeweza kupatikana.

"Kukosekana kwa Djuma si sababu ya sisi kwenda suluhu na Ndanda, katika mchezo wa mpira kunakuwa na aina ya matokeo matatu, sidhani kama wanaotupia lawama suala la yeye kubakia Dar es Salaam wanafanya jambo jema" alisema.

Ofisa huyo ameeleza kuwa Djuma alisalia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na majukumu ya kazi kwa kuwanoa wachezaji ambao hawakuambatana na kikosi kuelekea Mtwara kwa ajili ya mechi hiyo.

11 COMMENTS:

  1. Achaporojo hoja zako azinamashiko hatachembe timu gani duniani inaweza Fanya jambo la hovyo kama simba mbona mnajiona mmefika simba niyawengi huo mpango wenu utaleta mpasuko mkubwa ndani yatimu tangulini timu ikasafuri bila kocha msaidizi hao wachezaji waliobaki dar walikua wanaandaliwa wakapambane nanani wakati kikosi kamilikilikua mtwara kwenyevita jiangalieni mjitathimin simba atunaga uvumiluvu kwenye maamuxi ya ovyo tunakuaga watu wa ovyo mnapofanya ovyo

    ReplyDelete
  2. UPUUZI MTUPU. WACHEZAJI WALIOBAKI HATA WENYEWE WANGEWEZA KUSIMAMIA MAZOEZI YAO KWA HIZO SIKU MBILI AMBAZO MAKOCHA WAPO MTWARA KUTOMJUMUISHA KOCHA MSAIDIZI KUNALETA TAFSIRI HIYO KWAMBA MAKOCHA HAWAELEWANI SASA INAWEZEKANA SIO KWELI LAKINI HIYO NDIYO TAFSIRI WATU WANAISEMA. MATAKWA YA WENGI NI KUMUONA DJUMA YUPO NA KOCHA MKUU NA WACHEZAJI TATIZO NINI WAFURAHISHENI MASHABIKI WENU HAKIKISHENI DJUMA YUPO BILA KUTABIRI MATOKEO. HEBU NIULIZE, INGETOKEA SIMBA NDIO IMECHEZA NA YANGA, DJUMA MMEMPUMZISHA VILE, SIMBA IKAFUNGWA, HIVI HUWEZI KUTABIRI HASIRA ZA MASHABIKI ZINGEKUWAJE? VIONGOZI LAZIMA MJUE HISIA ZA MASHABIKI WENU ILI KUEPUSHA MIGOGORO INAYOWEZA KUEPUKIKA.

    ReplyDelete
  3. Huyo kocha Wa simba yatakiwa akubali kujishusha ili kuijua vizuri ligi ya Tanzania na c kukurupuka na kujiona kila kitu anakijua

    ReplyDelete
  4. Mia 3:5:2 ya masoud imetulia ila ya mbeligiji haijaeleweka kama ni matakwa ya Mo basi nae amekuja kupoteza muda na uwekezaji wake Mwl Mkuu ni mradi wa mtu

    ReplyDelete
  5. Katika hali ya kawaida, angebaki kocha wa viungo dar, ili hao wachezaj wachache wafanye mazoez madgmadg ya viungo, coz hawatoshi hata full game! Sasa mkafnya opposite.Hope halitajirudia

    ReplyDelete
  6. Mimi kama masoud ataachwa hata uanachama nauacha nimekasirika sana.simba hii siyo ya kutoka suluhu na ndanda. Kocha mzungu hana lolote. Si bora hats kuponovic aliyekuwaga na matola? Analipwa hela kibao bila sababu

    ReplyDelete
  7. Napingana na maelezo ya uongozi, suala la kuweka wachezaji fiti ni la kocha wa viungo sio kocha msaidizi. Kocha msaidizi ni mshauri mkuu wa Kocha Mkuu katika mechi, iweje awekwe pembeni katika mechi ambayo watu wanataka matokeo, acheni siasa katika soka bhana, MO amefanya uwekeaji mkubwa sana hapo. Timu imecheza mpira wa hovyo sana Mtwara

    ReplyDelete
  8. Mm ni simba damu ila ipigwe tuu kwa sababu viongozi wanazingua.Mnamyumbisha kocha aliyeleta heshima msimbazi mnamwamini huyo mzungu mwenye maneno mengi lakini matokeo ccmizi..hovyo kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic