September 5, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba umeendelea kuweka mkazo juu ya katiba itakayotumika katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba 3 2018.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Lyamwike, amesema kuwa katiba itakayohusika ni ya 2018 pekee na si vinginevyo.

Lyamwike ameamua kuweka msisitizo huo kutokana na baadhi ya wanachama kuendelea kuhoji juu ya katiba hiyo ambayo baadhi wanadai inawabana kwa baadhi ya vipengele haswa katika ngazi za elimu.

Wanachama hao baadhi walianza kuilalamikia katiba wakitaka kiwango cha elimu kwa mgombea Urais kiwe katika ngazi ya elimu ya kidato cha nne badala ya shahada kutoka chuo kikuu.

Simba walifanya mabadiliko kadhaa ya katiba hiyo na kusajiliwa na Msajili Mkuu wa Vyama vya Michezo ambaye pia alisema itatumika kwa shughuli zote za klabu ukiachana na ile ya zamani.

Tayari mchakato wa kuanza kuchukua fomu klabuni hapo upo wazi ingawa mpaka jana hakukuwa na mwanachama yoyote aliyejitokeza makao makuu ya klabu hiyo kuhitaji fomu hizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic