September 5, 2018


Mwanamuziki mwenye jina kubwa kwenye gemu la Hip Hop Bongo, John Simon ‘Joh Makini’ amesema kwamba kilichomfanya kuimba Gospo ni kufikisha ujumbe kwa mashabiki zake kwa namna Mungu anavyomaanisha kwenye maisha yake.

Akichonga na Risasi Vibes, Joh Makini alisema kwamba wimbo huo kwake ni ‘Hip Hop Gospo’ wenye ujumbe ‘strong’ na si mwisho wa kuimba nyimbo za namna hiyo, ataendelea kila anapopata idea kwa sababu Mungu ni kila kitu kwake.

“Hakuna ambaye hafahamu kwamba Mungu ni kila kitu kwenye maisha ya binadamu, nimeimba wimbo huu ili kufikisha ujumbe kwa mashabiki zangu kufahamu kwamba suala la Mungu kutufanikisha kwenye maisha yetu si la kumwachia yeye tu. 

“Sisi pia tunatakiwa kupambana kwa namna zetu nay eye anabariki nia zetu na kufanya tupate kila tunachotamani,” alimaliza Joh Makini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic