September 23, 2018

1 COMMENTS:

  1. Tunajua serikali ina mambo mengi ya kufanya lakini katika suala ambalo pia inatakiwa kulipa uzito wa aina yake basi ni ujenzi wa viwanja cha michezo hasa vya mpira wa miguu. Angalau kwa kila mkoa kukawa na kiwanja kimoja bora. Kwa kiasi fulani ni suala la serikali za mikoa kuhakikisha kila mkoa unakuwa na uwanja wake wa mkoa. Baharesa tajiri na Mungu amzidishie neema zaidi nasema kwa roho safi kabisa lakini hukaa na kujiuliza watendaji wetu wote ambao wengi wao ni wasomi wa fani mbali mbali kuna wachumi, mainjinia,mabwana shamba nk wanaohudumu kutoka ngazi ngazi mbali mbali za mikoa kwanini wanashindwa kuwa na angalau akili robo ya Baharesa katika kuleta maendeleo katika mikoa yao? Nadhani wazo la kila mkoa kusubiri maendeleo kutoka serikali kuu ni ukosefu wa akili na tutachelewa sana. Unaona kabisa hata kunako ile ajali ya mv Nyerere Mkoa ulikuwa hauko tayari kukabiana maafa ya ajali kama ile kutokana na upungufu zana za uokoaji kana kwamba walikuwa wanasubiri zana hizo zitoke Daresalam? Kunatakikana kuwe na mikakati maalum nchini kuhakikisha viongozi wa mikoa wanabeba misalaba zaidi katika kuiletea maendeleo mikoa yao badala ya kusubiri kila kitu kutoka serikali kuu. Vyoo vya wanafunzi ni kusubiri serikali kuu, kituo kidogo cha afya ni kusubiri serikali kuu,ukosefu wa madarasa kwa wanafunzi serikali kuu kwa kweli nchi haiwezi kupiga hatua kwa namna hiyo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic