September 23, 2018


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond Plutnumz’ usiku wa kuamkia leo amemuandikia mzazi mwenzie  Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ujumbe mzito katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Diamond amesema ataendelea kumheshimu Zari kwani amemzalia watoto wawili kwake yeye anaona kuwa ni jambo kubwa sana na zawadi iliyo njema.

“Hii ni siku muhimu sana kwako mama watoto wangu, Nashukuru kwa kunizawadia watoto wawili wazuri sana na kikubwa zaidi umekuwa mama mwema unawalea watoto vizuri.“amendika Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram na kueleza hisia zake zaidi.

“Niamini mimi, nitaendelea kukuheshimu daima ndio maana hauji kusikia nikikuzungumzia hovyo kwenye interview zangu ninazofanya, sio hivyo tu hata kuzungumzia chanzo cha mfarakano wa mapenzi yetu kamwe siwezi, watoto wetu tuliojaaliwa ni zawadi tosha kwangu,. Nitaendelea kukupenda, kukuheshimu na kukuchukulia kama dada yangu wa damu.“amemaliza Diamond Platnumz.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic