September 3, 2018


Kampuni ya Kubashiri ya Biko kwa kushirikiana na Kundi la WCB lililopo Chini ya Mbongo Fleva, Diamond Platnumz wamezindua rasmi mashindano ya ‘Jibebe Challenge’ yatakayokuwa yanafanyika kila siku ya Jumapili katika ukumbi wa The Life Club uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo ya Kucheza yameanzishwa siku chache baada ya Diamond, Lavalava na Mbosso kuachiwa wimbo wao wa Jibebe ambao umekuwa gumzo sana mjini.

Kama wewe ni kijana na una kipaji cha kucheza wimbo wa Jibebe basi fika kila Jumapili katika ukumbi wa Life Club ili uweze kushiriki katika shindano hilo na ikiwa ni bahati yako basi unaweza kusajiliwa WCB kwani wanahitai madansa kwa ajili ya Lavalava na Mbosso.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic