September 22, 2018


Na George Mganga

Wakati Yanga inaelekea kucheza mechi na Singida United Jumapili ya wiki hii, unaambiwa wapinzani wao wamezidi kuwa kwenye hali tete baada ya kuondokewa na Makocha wao wasaidizi.

Taarifa zinaeleza makocha hao ambao ni Jumanne Chale pamoja na Mfaume Athuman, wameachia ngazi kwa kile kinachoelezwa timu hiyo kukabiliwa na ukata wa fedha.

Makocha hao wameachia ngazi kwa kudai stahiki zao ikiwemo fedha za mishahara jambo ambalo limesababisha waondoke.

Timu hiyo imekabiliwa na changamoto ya ukata ikikumbukwa hivi karibuni kipa wake, Manyika Peter naye aliondoka kambini na kurejea Dar es Salaam kwenye kituo cha soka cha baba yake kuendelea kujifua.

Ukiachana na Manyika, inaelezwa pia mchezaji wake wa kimataifa Shafik Batambuze naye hajacheza mechi yoyote msimu huu akidai fedha zake za mshahara.

Singida itakuwa ina kibarua kizito dhidi ya Yanga Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mechi ikianza majira ya saa 1 za usiku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic