September 22, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umegomea mabadiliko mapya ya Bodi ya Ligi juu ya kubadilishiwa ratiba ya mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania uliopaswa uchezwe Septemba 26.

Yanga wameeleza kuwa hawakutuma maombi kwenda kwa ajili ya kusogezewa mechi hiyo mbele kwa kuwa wana muda mzuri wa kujiandaa kuelekea mechi dhidi ya Simba.

Mabingwa hao wa kihitoria katika Ligi Kuu Bara wamesema kama Simba walituma maombi ya kubadilishiwa ratiba basi ingekuwa vema wakabadilishiwa wao pekee na si kuwahusisha Yanga ambao hawakutuma.

Bodi ya Ligi kupitia TFF iliufanyia mabadiliko mchezo wa Yanga dhidi ya JKT Tanzania ambao ulipaswa kupigwa Septemba 26 na ule wa Simnba dhidi ya Biashara United uliopaswa kupigwa Septemba 27.

Mechi hizo sasa hazitofanyika tena mpaka pale bodi itakapopanga tarehe zingine.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic