September 16, 2018


Na George Mganga

Dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu Bara baina ya Yanga na Stand United umemalizikwa kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 4-3.

Mechi hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeshuhudiwa mabao ya Yanga yakikwekwa kimiani na Mrisho Khalfan Ngassa, Andrew Vincent na Deus Kaseke.

Wakati huo mabao matatu ya Stand United 'Hat Trick' yamewekwa kimiani na Alex Kitenge ambaye ameondoka na mpira.

Ushindi huo kwa Yanga unawafanya kufikisha jumla ya alama 6 sawa na Stand United United iliyopoteza.

Wakati huo huo Mbeya City iliyokuwa Uwanja wake wa nyumbani ikicheza na Alliance School ya Mwanza imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mbeya City wamejipatia mabao hayo kupitia kwa Victor Hanganya na Eliud Ambokile.

5 COMMENTS:

  1. Kitathmini Simba bado ana timu nzuri sana kulinganisha na yanga. Katika mechi mbili beki ya yanga imesharuhusu magoli manne na katika mechi tatu beki ya Simba haijaruhusu hata goli moja. Kitu ambacho watu wengi wanaiangalia Simba kwa ubora wa washambuliaji wake na watu wengi wakiuzungumzia Simba kuwa na beki dhaifu lakini takwimu siku zote
    hazidanganyi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hawajaruhusu bao, lakini wamefunga mangapi!? Issue in kuwa simba wana timu nzuri Ila wanatumia muda mwingi kujilinda kuliko kushambulia!! Yanga wanashambulia zaidi na ndio maana game mbili bao sita!time haishindi kwa kujilinda Bali kwa kushambulia

      Delete
  2. Km huna la kuongea nyamaza c lzm uitaje hiyo mbumbumbu fc

    ReplyDelete
  3. yanga hongereni sana japo mmewhinda kwa mbinde

    ReplyDelete
  4. Yanga chupuchupu at home

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic