September 18, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuruhusu kambani mabao matatu kutoka kwa straika hatari wa Stand United, uongozi wa Yanga umemkingia kifua kipa wake, Mkongomani, Klaus Kindoki kwa kusema hana makposa yoyote.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano, Hussein Nyika, amesema kuwa kilichotokea juzi Uwanjani ni matokeo ya mpira hivyo hakuna haja ya kumtupia lawama Kindoki.

Nyika ametolea ufafanuzi suala la mashabiki wengi wa Yanga kuutaka uongozi umuweke benchi kipa huyo kuwa halina mantiki kwa maana matokeo hayo yametokana na namna timu mbili zilivyocheza.

Kiongozi huyo amefunguka kuwa timu ilikuwa uwanjani kwa lengo la kusaka pointi tatu ambapo lengo hilo lilifanikiwa, akieleza si vema kuanza kumtupia lawama kipa wao.

Aidha, Nyika amesema kama mchezaji alifanya makosa si sahihi kuwekwa benchi na badala yake Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera kama mkuu wa benchi la ufundi atarekebisha mapungufu ya kikosi.

Kauli hiyo inakuwa inatoa jibu moja kwa moja kwa baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao walianza kuutaka uongozi kumpiga benchi kipa huyo wakidai aliruhusu mabao kiulaini.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi Jumapili, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-3 ambayo yalifungwa na Mrisho Ngassa, Ibrahim Ajibu, Andrew Vincent na Deus Kaseke.

6 COMMENTS:

  1. Vipi makali ya Makambo naona hakutia goli na yeye ndie alietabiriwa namba one kwa kuchana nyamvu. Ajitazame vizuri kabla hajatakiwa kukaa benchi na huyo kipa anaekataliwa si kaletwa na Zahera mwenyewe na jee mechi hiyo ingechezwa ugenini ingekuwaaje?+

    ReplyDelete
  2. Huyo kipa mzembe sana, hapangi beki, hatoki golini, hachezi klosi. Kakaa tu kama mzigo golini. Anatetemeka kama vle ni Mara ya kwanza kukaa golini. Katuaibisha sana wanayanga

    ReplyDelete
  3. Huyo kipa mzembe sana, hapangi beki, hatoki golini, hachezi klosi. Kakaa tu kama mzigo golini. Anatetemeka kama vle ni Mara ya kwanza kukaa golini. Katuaibisha sana wanayanga

    ReplyDelete
  4. Wewe nyika unatuzingua unasajili wachezaji wa bei poa ili upige cha juu. Kwani club haina msemaji mpka ujibu wewe? Dismass kazi yake nn? Acheni kutuchezea wanayanga kwa kutaka kujaza tumbo lako pesa za wanayanga. Wenzako waliondoka why wewe ung'ang'anie? Ole tufungwe hiyo sept 30 uje na majibu ya kitoto kama haya.

    ReplyDelete
  5. Wewe nyika unatuzingua unasajili wachezaji wa bei poa ili upige cha juu. Kwani club haina msemaji mpka ujibu wewe? Dismass kazi yake nn? Acheni kutuchezea wanayanga kwa kutaka kujaza tumbo lako pesa za wanayanga. Wenzako waliondoka why wewe ung'ang'anie? Ole tufungwe hiyo sept 30 uje na majibu ya kitoto kama haya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mnyika hana hadhi ya kumjibia golikipa Hugo.Kwani kama ni yeye mwenyekiti wa usajili ameyumia Pesa za Yanga za kutosha sana kwendà kulileta kokoro ambslo linawachosha mabeki wake,Kwa uzembe wake.Basis hill koti analomfunika kipa Hugo linasaidia tu kuficha ulaaji wake Kwa mgongo Wa kipa huyo basi sisi wapenzi Wa Yanga tunalivua koti hill hadharani.tunakuambia tuondolee kokoto hill.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic