October 11, 2018


Uongozi wa timu ya Alliance umejipanga vilivyo kuelekea mechi yake na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa Oktoba 20 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Alliance wamesema kuwa wameshaanza maandalizi ya moto kuelekea mechi hiyo ambayo wametamba kuweka historia jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa timu hiyo, Jackson Mwafulango, amesema wamejipanga kuifunga Yanga iki kuweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kuchukua alama tatu za Yanga msimu huu.

Mafulango amejigamba kuwa watakuja na moto wa aina yake ili kuwashangaza wengi ambao wanaichukulia timu hiyo kuwa ni ya kawaida.

"Tumeshaanza maandalizi muda na tunataka kuja kuondoka na alama tatu dhidi ya Yanga OktobA 20, tumedhamiria kuweka rekodi ya kuondoka na alama hizo ili kuweka rekodi ya kuwafunga Yanga msimu huu" alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic