October 15, 2018



GULLAM DEWJI...



Baba mzazi wa Mohamed Dewji anatarajia kuzungumza leo kuhusiana na tukio la kutekwa kwa mwanaye.

Taarifa zimeeleza, Gullam Dewji atazungumza na wanahabari leo kwenye ofisi za Kampuni ya MeTL katika jengo la Golden Jubilee katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Mwananchi imemnukuu Gullam Dewji ambaye ni mwanzilishi wa kampuni ya MeTL akithibitisha kwamba atazungumza leo Saa 6:30 mchana.

Ofisi hizo pia hutumiwa na Mo Dewji ambaye alitekwa Alhamisi ya Oktoba 11, 2018 wakati akiingia gym kwa ajili ya mazoezi katika hoteli ya Collosseum.

Vyombo vya kiusalama vimekuwa vikiendelea na kazi ya kuhakikisha Mo Dewji anapatikana na wananchi wamekuwa wakiombwa kutoa ushirikiano kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na wahalifu ambao wameelezwa kuwa ni raia wa kigeni, wanapatikana mara moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic