October 15, 2018




Straika mpya wa Azam FC, Donald Ngoma, raia wa Zimbabwe, ameweka wazi kuwa kufunga ni kawaida yake na ataendelea kutupia mabao zaidi kwenye mechi zao.

Ngoma alifunga bao lake la kwanza akiwa na jezi za Azam wiki chache zilizopita ikiwa ni baada ya kupita kwa zaidi ya miezi 10 ambayo alikuwa nje akiuguza majeraha ya nyama za paja.

Mzimbabwe huyo alifunga bao hilo katika ushindi walioupata Azam wa mabao 2-0 mbele ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.

Ngoma alisema kuwa kwake anajisikia vizuri kufungua ukurasa wa mabao ndani ya timu hiyo huku akiweka bayana kwamba kwake kitu cha muhimu ni klabu yake ipate ushindi.

“Kwangu kufunga ni kitu cha kawaida, nimefurahi sana kwa sababu tumepata pointi tatu na ndiyo muhimu sana.


“Ukiwa straika kufunga ndiyo kazi yako ya kwanza na nimefurahi sana kwa sababu ni timu yangu mpya na nimeanza kuifungia,” alisema. 





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic