Beki mkabaji wa timu ya Yanga ambaye anakubalika na mashabiki kutokana na uwezo wake Uwanjani licha ya kupandishwa kutoka kwenye timu ya vijana, Paul Godfery amesema kuwa Yanga kwake ni njia ya kwenda Ulaya.
Godfrey amefiti kwenye nafasi ya nahodha msaidizi Juma Abdul ambaye amekuwa nje kutokana na majeraha amesema kuwa anapenda kwenda kucheza ulaya hali inayomfanya azidi kuongeza juhudi kila siku.
"Ligi ni ngumu na ninazidi kujifunza kila siku nikiwa ndani ya Yanga, ushirikiano ninaoupata kutoka kwa wachezaji na mwalimu unazidi kunipa nguvu, malengo yangu kuweza kucheza soka la kulipwa nje,nitapambana kufikia malengo niliyojiwekea," alisema.
Godfrey katika mchezo wao uliopita dhidi ya KMC alifanikiwa kupiga mashuti makali matatu ambayo yote yaligonga mwamba, amekuwa chini ya uangalizi wa uongozi wa Yanga ili aendelee kubaki katika kiwango chake.
0 COMMENTS:
Post a Comment