Pambano la Ligi Kuu Bara kati ya KMC na Yanga lililopigwa Uwanja wa Taifa, Alhamisi limeacha rekodi ya aina yake baaada ya timu hizo kumaliza dakika 90 bila kupigwa kona hata moja.
Yanga waliibuka kidedea dakika ya 89 kwa kufunga bao 1-0 , timu zote zilicheza kwa mbinu ya kupiga pasi za chini lilimalizika kwa kuweka rekodi hiyo ya kutopatikana kwa kona katika mechi zilichezwa hivi karibuni Taifa kwa kuwa zilikuwa na kona.
Mchezaji wa zamani wa Yanga Mohamed Hussen 'Chinga' amesema kuwa kitaalamu inatokana na umakini wa beki kuweza kuzuia mashambulizi pamoja na udhaifu wa safu ya ushambuliaji.
"Kona inamaanisha mashambulizi yamezidi kwenye lango la mpinzani, kama hakuna kona inamaanisha kuwa beki ilikuwa imara kuzuia washambuliaji kufika eneo la hatari, wakati mwingine inachangiwa na safu ya ushambuliaji kutokuwa makini," alisema.
post ya kijinga
ReplyDeleteAcha kuongea matapishi nyie tunawajua Kazi kupaki basi mpira hamujua mupo tu kwa bahati ya mwenyezi mungu
ReplyDelete