EMMANUEL Okwi na Claytous Chama jana walifanikiwa kuipa
ushindi Simba wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar, na kuufanya mji kuwa kimya kutokana na kuzima kelele za Yanga.
Ushindi huo
wa Simba umetokana na mabao ya Chama dakika ya 30 na Okwi dakika ya 45 ikiwa ni
muda mfupi kabla ya timu hazijaenda mapumziko.
Eric Mulilo alijifunga dakika ya
77 na kuhitimisha ushindi
huo mnono wa Simba. Ushindi huo umejibu ushindi ambao Yanga
iliupata juzi baada ya kuifunga Alliance 3-0 kwenye uwanja huohuo.
Katika
mchezo huo wa Ligi Kuu Bara jana Jumapili, Simba ilionekana kuwa na shauku
kubwa ya kuondoka na ushindi kwani muda mwingi ilikuwa ikilishambulia lango la
Stand United.
Juhudi zao hizo walizoanza kuzionyesha tangu mwanzo wa mchezo,
zilizaa matunda kwa mabao hayo ya kideoni yaliyofugwa kwa ustadi wa hali ya
juu.
Hata hivyo, wachezaji wa kikosi hicho akiwemo Kagere, Okwi, Shiza Kichuya
na wengineo, wanatakiwa kujilaumu kutokana
na kukosa nafasi nyingi za wazi za kufunga mabao.
Simba
imepata ushindi huo ikiwa ni siku chache baada ya Yanga kuifunga Alliance mabao
3-0 uwanjani hapo ambapo mashabiki wao walianza kusumbua mjini, lakini sasa
kelele zao zimezimwa kutokana na idadi hiyo ya mabao kulipwa.
Ushindi huo
umeifanya Simba kufikisha pointi 17 ikikamata nafasi ya tatu nyuma ya Yanga
yenye pointi 19. Kinara ni Azam yenye pointi 21. Simba imecheza mechi nane,
Yanga saba, Azam tisa.
Matokeo ya mechi nyingine; Mbao 1-0, mfungaji Said
Khamis dakika ya 48, na katika mchezo wa awali Lipuli 0-1 Kagera.
hii habari umeisoma kabla ya kuiposti kweli?
ReplyDeleteJana simba kacheza name stend au YANGA....au ndo kuuza habari?