Meneja wa Yanga ambao ni mabingwa wa kihistoria Ligi Kuu Tanzania Bara, Nadir Haroub 'Canavarro" amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya Lipuli FC.
Yanga itacheza mchezo wake wa 9, Uwanja wa Taifa. baada ya kufanya vizuri kwenye michezo yao 8 iliyopita, wamefanikiwa kushinda michezo saba na kutoa sare mchezo mmoja.
"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Lipuli maandalizi asilimia kubwa yamekamilika, wachezaji wana morali kubwa ya kucheza na mwalimu amewapa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kupata matokeo.
"Hali ya Ibrahim Ajibu, Papy Tshishimbi zimetengamaa hivyo daktari anasubiriwa ili kutoa ruhusa kama mwalimu anaweza kuwatumia," alisema.
Ajibu alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya mgongo aliyoyapata katika mchezo wake dhidi ya Alliance, Tshishimbi naye alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya fundo la mguu, walioukosa mchezo uliopita dhidi ya KMC ambao Yanga walishinda kwa bao 1-0.
Wampe elimu makambo, apambane maana mpira wa miguu ni mapambano siyo anarukaruka tu kama mcheza masebene
ReplyDelete