October 29, 2018


Mshambuliaji nyota wa timu ya Simba raia wa Uganda ,Emmanuel Okwi amesema kuwa licha ya kupata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Ruvu Shooting mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa, bado walikuwa na nafasi ya kufunga mabao mengi ila safu ya ushambuliaji haikuwa makini.

Okwi msimu uliopita alifunga mabao 20 na kuibuka na tuzo ya mfungaji bora, alipewa zawadi ya shilingi Milioni tatu, ameanza kuonyesha makali yake baada ya Simba kucheza michezo 10 amefanikiwa kufikisha jumla ya mabao 7.

"Namshukuru Mungu tumefanikiwa kushinda nami nimefanikiwa kupiga 'Hat-trick' imewezekana kwa sababu ya ushirikiano mzuri uliopo ndani ya timu hivyo peke yangu nisingeweza kufika hapa.

"Tumetengeneza nafasi nyingi tumeshindwa kufunga kwa sababu tulikosa utulivu tulipokuwa ndani ya eneo la hatari, ila ni makosa ambayo yapo tumeyagundua tutayafanyia kazi bado tuna mechi nyingi tutaendelea kufunga." alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic