October 9, 2018


Kutokana na Simba kutengeneza nafasi nyingi katika mechi wanazocheza ligi kuu na kushindwa kuzitumia vizuri, Kocha Mkuu wa Simba, raia wa Ubelgiji, Patrick Aussems, amesema kuwa anahitaji wiki mbili kuweza kusuka kikosi bora.

Simba wamecheza mechi 7 huku wakiwa na idadi ya mabao ya kufunga nane huku wakifungwa mabao matatu, licha ya kuwa na washambuliaji wengi wa kimataifa jambo ambalo kocha mkuu halimfurahishi.

Aussems alisema kuwa kikosi cha Simba ni kipana na kina wachezaji wengi wazuri ambao wanahitaji kuongezewa ujuzi zaidi na kuweza kuwafanya wacheze kwa kuelewana hasa katika safu ya ushambuliaji.

“Tuna wachezaji wengi wazuri ambao wanahitaji kupewa ujuzi zaidi, hasa wa kutumia nafasi ambazo wanazipata katika mashindano ambayo tunashiriki, hivyo baada ya kukaa nao kwa muda wa wiki mbili, ninaamini nitakuwa na kikosi kizuri.

“Kwa sasa nina wachezaji kama akina Salamba (Adam), Niyozima (Haruna) ambao wanaweza kufanya mambo makubwa kwenye timu ila ni jambo la kusubiri tu wakati ili waweze kuwa katika ubora wao, taratibu tunaanza kuondoka kwenye tatizo la kutumia nafasi, hatuwezi kutoka ghafla tu, linahitaji muda,” alisema Aussems.

9 COMMENTS:

  1. tu hivi wachezaji wa nje wanaoruhusiwa kusajiliwa na vilabu ni saba (7) au tisa (9) maana naona Simba wamesajili wachezaji tisa (9) !!!!!

    ReplyDelete
  2. Wacha ushamba ulikuwa hela nini?Hujui kwamba kanuni zimebadilishwa inaruhusiwa kusajili wachezaji 10 wa kigeni?
    Au ulikuwa umelala sasa ndio umezinduka usingizini?

    ReplyDelete
  3. Ulikuwa jela na leo ndio umetoka?Kanuni zimebadilishwa.

    ReplyDelete
  4. Kata rufaa. Ni kweli Simba imesajili wachezaji 9 wa kigeni .Jamaa kakurupuka kutoka kwenye coma. Ni 2018.

    ReplyDelete
  5. Hamjui kujibu kistaarabu hadi urushe maneno au ndivyo mlivyolelewa !!

    ReplyDelete
  6. Umejibiwa ulivyouliza. Waliokujibu hawana makosa. Ulikurupuka ukajibiwa.

    ReplyDelete
  7. sidhani kama majibu ya kejeli ndio maadili yetu watanzania !!
    kwa taarifa ya walionikejeli ni kua mimi naishi nje ya Tanzania na sifuatilii habari za michezo kila siku na ndio sababu nikauliza kama ni saba au tisa na wala sijalaumu mtu bali niliuliza ili kujua !!
    sasa huko kutoka jela au kwenye coma au ushamba au kukurupuka kumetokea wapi !!

    ReplyDelete
  8. Jamaa yupo nje ya Tanzania na hakuwa na Internet kwa hiyo amepitwa na mengi.Sasa ndio anafanya catching up.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic