October 7, 2018


Kikosi cha Yanga kesho kinashuka dimbani kukipiga na wababe wa Simba, Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kuelekea mechi hiyo, uongozi wa Yanga umesema utamkosa mchezaji wake Juma Mahadhi ambaye bado anaumwa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema Mahadhi atakosekana kutokana na kuendelea kuuguza majeraha yake.

Kwa upande wa maandalizi Ten ameeleza kuwa wamejiandaa vema tayari kuchuana na Mbao ambao waliwafunga watani zao wa jadi Simba jijini Mwanza hivi karibuni.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 1 kamili za usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

2 COMMENTS:

  1. Hilo neno wababe linatoka wapi kat ya yanga na simba nani kibonde kwa mbao? Acha kuharb habar ww

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic