October 7, 2018


Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hatimaye kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya amefanikiwa kufunga bao la kwanza.

Kichuya alifunga bao hilo mnamo dakika ya 9 ya mchezo na kuweka rekodi yake msimu huu kupachika bao la kwanza baada ya ukame tangu kuanza kwa mechi za msimu huu.

Mbali na Kichuya, straika mganda, Emmanuel Okwi naye alifanikiwa kupasia kamba kwa mara ya kwanza.

Okwi alicheka na nyavu kwa mpira wa kichwa mnamo dakika ya 48 kipindi cha pili na kufanya matokeo kuwa mabao 2-1.

Okwi na Kichuya wamefanikiwa kucheka na nyavu ikiwa ni baada ya mechi 6 bila kufunga.

Katika mchezo huo bao la kufutia machozi kwa African Lyon liliwekwa kimiani na Awadh Juma kwenye dakika ya 62 alilofungwa kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la 18.

3 COMMENTS:

  1. Nimeshangaa sana TZ1 kufungua goli la mbali kama lile,kaka kaa vizuri Kalokonya anakuja vizuri wachukia TZ1 sio muda mrefu

    ReplyDelete
  2. Kabla yabkushangaa unatakiwa kumsifu kwanza mpigaji, mimi mwenyewe ni simba damu lakini nililipigia makofi goli lile. Pale ukichukua magolikipa 10 bora wa dunia si ajabu watano wangefungwa goli la namna ile. Ni goli bora.

    ReplyDelete
  3. Hilo goli kwakwel ni zuri jamaa kafunga wala msimlaum kipa kwan kipa hakai sehem moja2 kipa mpira unapopgwa jaman hii ni soka inamaajab yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic