October 27, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kama mshambuliaji wake Amissi Tambwe anataka kucheza kikosi cha kwanza anatakiwa afike kiwango cha Meddie Kagere wa Simba.

Zahera alisema Tambwe wa misimu miwili iliyopita siyo huyu wa sasa kwani kasi yake imepungua ndani ya uwanja kutokana na kuongezeka uzito baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

"Zamani Tambwe alikuwa anaweza kukimbia kilomita 30, sasa hivi anakimbia kilomita 10 kutokana na kusumbuliwa na majeraha muda mrefu hali iliyofanya kasi kupungua na nimekuwa nikimshauri kubadilika, ninamtaka awe na kasi kama Kagere wa Simba," alisema.

Tambwe amewahi kuwa mfungaji bora mara mbili Ligi Kuu Bara akiwa Simba 2013/14 na Yanga 2015/16, mpaka sasa ana mabao 2 tu aliyoyafunga katika mchezo wao dhidi ya Singida United. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic