October 17, 2018



UNAWEZA kusema mambo ni mazuri kwa upande wa kipa wa Yanga, Beno Kakolanya ambaye mpaka sasa anaonekana kumkimbiza kipa wa Simba, Aisha Manula kutokana na kuwa na takwimu bora kwenye ligi.

Kipa huyo wa Yanga amecheza jumla ya dakika 329 na kuruhusu bao moja pekee ambalo alifungwa katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao walishinda mabao 2-1. 


Yanga imefanikiwa kucheza mechi sita na aliweza kudaka mechi nne dhidi ya Simba (0-0), Singida United (2-0), Mtibwa Sugar (2-1) na ule dhidi ya Mbao FC, ambao alidaka mpaka dakika 59 alitoka baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Klaus Kindoki. 


Timu hiyo imecheza mechi sita na kufunga mabao 11 na kuruhusu mabao manne moja la Beno na matatu ya Kindoki. 


Kwa upande wa Manula ambaye msimu uliopita ndiyo aliibuka kuwa kipa bora kwa mara ya pili mfululizo kwenye kikosi chake wamecheza mechi saba na zote amedaka mwenyewe. 


Katika mechi hizo saba ameruhusu mabao matatu, ambayo alifungwa kwenye mchezo wao dhidi ya Mbao FC (0-1), Mwadui FC (1-3) na African Lyon (2-1). 


Mechi nyingine ambazo Simba imecheza ni dhidi ya Tanzania Prisons (1-0), Mbeya City (2-0) Yanga (0-0) na Ndanda FC (0-0). 


Msimu uliopita ligi ilipomalizika Manula katika mechi 29 aliweza kuruhusu mabao 14 ambayo ndiyo yalikuwa machache kwenye ligi huku Kakolanya msimu uliopita hakuwa na nafasi ndani ya kikosi chake. 


Ukiachana na michezo ya ligi, Manula aliruhusu pia bao moja kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, wakati Simba ilipovaana na Mtibwa Sugar na kuibuka na ushindi wa bao 2-1. 


Hata hivyo, Manula pia amesharuhusu mabao matatu kwenye michezo miwili ya timu ya Taifa, huku Kakolanya akikaa nje, hii inaonyesha kuwa kipa huyo wa zamani wa Azam amesharuhusu mabao saba kwa msimu huu hadi sasa.

8 COMMENTS:

  1. Kulinganisha kijinga sana. Kwa hiyo kipa aliyecheza mchezo mmoja kwa mfano na kutoruhusu bao atakuwa bora kuliko aliyecheza mechi 10 na kuruhusu mabao 6?Ukanjanja huu wa kulinganisha ni wa kijinga sana.Anayecheza anajulikana na anayekaa benchi anajulikana.

    ReplyDelete
  2. Dah! Uchambuzi uchwara, ulinganisho uendane na idadi ya mechi na aina za mechi ni za ushindani was kiasi gani! Sawa Kakolanya ni mzuri lakini si kwa Manula!!

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Ameruhusu, mabao timu ya taifa?. Ungepeleka kipa wako ambaye hawezi kuruhusu mabao. mabeki wapigwe chenga waanguke, unataka kipa azuie vipi goli la namna hiyo?

    ReplyDelete
  5. kakolanya ni bora kuliko manula ila kwa ushabiki wa kijinga watu mnasema manula ndo bora, angalieni magoli anayofungwa manula ndipo mjue manula ni bora au amechoka

    ReplyDelete
  6. Yale magoli ya hat trick hats angekaa beno angechapwa tu maana katika kufungwa kuna mawili au matatu uzembe wa kipa,uzembe wa mabeki,au kuzidiwa kwa namna yoyote ile,katika mpira kuna watu hata ukabe vp wanakuchapa tu yani kazikazi mwanzo mwisho sasa mpira waliocheza yanga siku ile mpaka wakatoka 4-3 ulikua mpira wa kipumbavu na magoli yalikua sio tatizo la kipa ni mabeki wazembe.

    ReplyDelete
  7. Yale magoli ya hat trick hats angekaa beno angechapwa tu maana katika kufungwa kuna mawili au matatu uzembe wa kipa,uzembe wa mabeki,au kuzidiwa kwa namna yoyote ile,katika mpira kuna watu hata ukabe vp wanakuchapa tu yani kazikazi mwanzo mwisho sasa mpira waliocheza yanga siku ile mpaka wakatoka 4-3 ulikua mpira wa kipumbavu na magoli yalikua sio tatizo la kipa ni mabeki wazembe.

    ReplyDelete
  8. Ha ha ha ha ha kwanza kuna wanao omba MO asipatikane kabisa,kwa staili hii hatuwezi kufika unamlinganisha mtu ambaye hajacheza mechi za nnje hata moja na T.O kweli???hata afanye nini hawezi kumfikia T.O AISHI MANULA,na ndiomana kwenye timu ya taifa kakolanya ataendelea kuchezea benchi sana.na kaa ukijua mpira ni dk90 sasa wewe ligi ndio kwanza hata mechi kumi bado mnabwata kama vile mlisha chukua kombe.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic