Bwire ambaye alisema kuwa ana kikosi makini ambacho kingempa matokeo chanya kwa kutambulisha mfumo mpya wa kupapas square mbele ya mabingwa watetezi Simba, dakika 90 zilipokamilika hakuonekana uwanjani.
"Sikukimbia waandishi wala mashabiki, kikubwa ambacho nilikuwa nakifanya ni kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine, nilitoka eneo la VIP, nikawafuata viongozi na mashabiki wangu ili kuimarisha hali ya usalama kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
"Tumefungwa kwa sababu ya washambuliaji kukosa umakini ila soka tumelionyesha,wapinzani wetu hawawezi kutupapasa kwa sababu ili upapase ni lazima uwe makini hasa katika kazi sasa sisi kufungwa haimaanishi hatuna uwezo," alisema.
Matokeo hayo yanaifanya Ruvu Shooting kushindwa kupanda kwenye nafasi za Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi zao 13 baada ya kucheza michezo 11.
0 COMMENTS:
Post a Comment