Kikosi cha timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC kimefanikiwa kutakata mbele ya wapinzani wao Ndanda FC, kutoka Mtwara baada ya kuwafunga mabao 3-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
KMC imepata ushindi huo baada ya kupoteza mchezo wake uliopita mbele ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0.
KMC walianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Omary Ramadhani dk ya 14, James Msuva akatupia dk ya 60 na kufanya hivyo tena dk ya 76.
Ushindi huo unakuwa ni wa 2 kwa KMC kwenye ligi baada ya kucheza michezo 12 huku wakiwa na sare 7 na jumla ya kupoteza michezo 3 wanafikisha pointi 13.
0 COMMENTS:
Post a Comment