October 31, 2018

Mmoja wa makocha wa Chelsea Marco Ianni amepigwa faini na Chama cha Soka cha England (FA) kutokana na alivyosherehekea bao la dakika za mwisho la klabu yake dhidi ya Manchester United.
Chelsea walifunga bao dakika ya 96 na kusawazisha na matokeo yakawa 2-2 katika mechi hiyo ya Ligi ya Premia iliyochezewa uwanjani Stamford Bridge wiki moja iliyopita.
Ianni alitimka mbio na kusherehekea mbele ya benchi la kiufundi la Manchester United, jambo ambalo lilimkera sana Jose Mourinho ambaye aliwahi kuwa meneja wa Chelsea kwa vipindi viwili awali.
Mourinho alinyanyuka mbio kutoka kwenye kiti chake na kuonekana kutaka kumfukuza kwa hasira lakini akazuiwa na walinzi uwanjani.
FA wamesema Ianni amekiri kosa la "utovu wa nidhamu" na amepigwa faini ya £6,000.
Mourinho hakuadhibiwa na FA kutokana na mchango wake katika vurugu zilizotokea, lakini "amekumbushwa rasmi kuhusu wajibu na majukumu yake
Mreno huyo alisema Jumattau kwamba Ianni alimuomba radhi kwa tukio hilo lililotokea 20 Oktoba baadaye.
"Ningependa kuwashukuru Chelsea na Maurizio Sarri - meneja wa sasa wa Chelsea," Mourinho alisema.
"Kijana huyu mdogo hahitaji adhabu zaidi ya aliyoipata.
"Aliniomba radhi. Anahitaji kusamehewa, hastahili kufutwa. Alipitia tukio ambalo mwenyewe anakubali kwamba alikuwa amekosea.
"Natumai kwamba kila mtu atafanya hivyo na asivuruge taaluma na jamaa huyu mzuri sana. Pengine ni mtu mwenye matumaini makubwa sana katika kazi hii. Sitafurahia kamwe hatua zaidi ya hizo zikichukuliwa."
Baada ya mechi, Mourinho aliinua vidole vitatu, ambao ulionekana kuwa ujumbe wa kuwakumbusha mashabiki wa Chelsea kuhusu vikombe vitatu vya ubingwa wa ligi alivyoshinda akiwa na Chelsea 2005, 2006 na 2015.
Baada ya mechi kumalizika, Maurizio Sarri, alisema alizungumza na Mourinho na alikiri kwamba mkufunzi huyo wa Chelsea ndiye aliyekuwa na makosa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic