October 31, 2018


Ligi kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja utakaochezwa Uwanja wa Uhuru kwa timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC kucheza na Ndanda FC kutoka Mtwara.

KMC walipoteza mchezo wao dhidi ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0, bao lilofungwa dakika za lala salama baada ya beki wa Ally Ally kumchezea rafu Herieter Makambo dakika ya 89, na kusababisha mwamuzi kuamua faulo iliyokwenda wavuni baada ya kupigwa na Fei Toto.

Kocha wa Ndanda, Malale Hamsini alisema kuwa wapo tayari kupambana kwa kuwa wachezaji wana morali kuhakikisha wanaweza kufanya vizuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic