October 21, 2018



KUNA taarifa kuwa siku za kocha wa Real Madrid, Julen Lopetegui kuinoa timu hiyo zinahesabika. 

Kocha huyo taarifa zinasema kuwa amepewa mechi tatu za kupata matokeo mazuri ili abakie katika kiti hicho. 



Real Madrid katika siku za karibuni imekuwa na mwenendo mbovu ambapo haijashinda mechi nne wala kufunga mabao. 



Lopetegui alitakiwa kupata matokeo mazuri dhidi ya Levante, ambayo walicheza nayo jana na ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Viktoria Plzen na dhidi ya wapinzani wa jadi, Barcelona
Hata hivyo, wakati Lopetegui amepewa hizo mechi tatu, kuna taarifa Real wamewasiliana na kocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte. 


Rais wa Real Madrid, Florentino Perez inadaiwa ameanza kuweweseka kutokana na kuyumba kwa timu hiyo.
Habari zinaeleza kuwa Lopetegui amepoteza imani ya wachezaji, ambapo kutokana na hali hiyo uongozi umeanza harakati za kusaka mbadala wake. 


Real Madrid inasemekana ilizungumza na Conte mwanzoni mwa msimu lakini kipindi hicho alikuwa katika majadiliano ya namna ya kuondoka Chelsea na alikuwa anafuatilia malipo yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic