October 21, 2018



Neymar ameshikwa mchecheto wa kuondoka PSG kutokana na kuhofia kufunikwa na Kylian Mbappe. 

Mbappe, ambaye aliisaidia Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia amekuwa moto pia katika Ligue 1.


Wachambuzi wa soka wanasema kuwa PSG imeweka bei ya pauni milioni 220 kwa timu itakayotaka kumsajili straika huyo.
Barcelona na Real Madrid zinatazamiwa kuingia katika vita kali ili kumnasa mkali huyo. 


Neymar amekaririwa hivi karibuni akidai kuwa anataka kurudi Barcelona na uongozi wa klabu hiyo unatafakari kumrudisha licha ya kuondoka kwake kusababisha mtafuruku mkubwa. 


Alikwenda mbali zaidi na kudai anajutia kuondoka Barcelona lakini watu wengi wanaamini presha ya Mbappe ndio inamsumbua.
Real Madrid ilitaka kumsajili mwanzoni mwa msimu huu lakini baadae ikabadili mawazo lakini kwa sasa ipo katika presha kubwa ya kumpata. 


Timu hiyo inayumba kufuatia kuhama kwa staa wao, Cristiano Ronaldo, ambapo imekuwa inakabiliwa na tatizo kubwa la ufungaji

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic