October 4, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amefichua kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusufu Manji amemueleza kwamba anarejea.

Kocha huyo mwenye uraia wa Ufaransa na DR Congo, wikiendi iliyopita aliiongoza Yanga kutoka suluhu na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Zahera amesema kuwa ameshakutana na kiongozi huyo mara tatu na kikubwa alichomueleza ni kurejea kwenye timu hiyo ingawa hajasema ni lini.

Zahera aliongeza kuwa hajui lini kiongozi huyo ataweza kurejea kama alivyoweza kumueleza kwa kuwa ni jukumu la mabosi wake wa juu, hivyo hawezi kuhusika nalo.

“Ndiyo (Manji) nimeshakutana naye zaidi ya mara tatu na anatoa ushauri wake kwenye timu vipi tufanye, kuhusu yeye kurudi hilo siyo jukumu langu lakini amekuwa akinieleza tu kwamba atarudi ila sijui lini kwa kuwa ni jambo la wakubwa wangu.

“Aliniambia anaweza kurejea Septemba, Novemba au Desemba ila sasa siwezi jua itakuwa lini,” alisema Zahera.
Manji alijiuzulu Yanga kwa kila alichodai kuwa anataka kuishughulikia afya yake lakini pia akasema anataka kwenda kupumzika.

Lakini kila siku imekuwa ik¬ielezwa kuwa mwenyekiti huyu mwenye ushawishi mkubwa anataka kurejea kwenye timu hiyo ingawa hawajawahi kuzungumza moja kwa moja kukiri au kukataa suala hilo.


4 COMMENTS:

  1. Hizo ni hadithi za Alfu Lela Ulela, hekaya za Hisopo

    ReplyDelete
  2. Kocha amekuwa msemaji wa Yanga kwani kila jambo yeye ndio msemaji .Mara Simba walituzidi mara tuliwaachia possesion. Mara alaumu wachezaji wake kwa kutofuata game plan.Mimi ni Yanga lakini kocha huyu anaanza kunipa wasiwasi.

    ReplyDelete
  3. MAMBO YA YANGA WAACHIENI YANGA WENYEWE, SIMBA SHUGHULIKENI NA MIPANGO YENU !!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic