October 10, 2018


Kutokana na timu yake kufanya vibaya katika Ligi Kuu England, Kocha wa Manchester United amezidi kuwashangaza wengi kwa kuendelea kukaa hotelini.

Mourinho ambaye ameingia kwenye tetesi kubwa za kufukuzwa kazi kutokana na aina ya mpira ambao United inacheza na matokeo, imeelezwa mpaka sasa hajachukua nyumba katika mji wa Manchester.

Maamuzi hayo ya Mourinho yanaelezwa kutokana na kujawa na hofu juu ya hatma yake na United akiamini muda wowote anaweza akaondoshwa.

Kocha huyo aliepuka kufukuzwa kibaruani kufuatia kupata ushindi wa mabao wa mbinde 3-2 dhidi ya Newcastle United kwenye Uwanja wa Old Trafford.

1 COMMENTS:

  1. Ishu sio kufukuzwa ila tangu day one amefika manchester aliamua kukaa hotel inaitwa Salford's Lowry Hotel, muache kupotosha watu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic