October 10, 2018


Baada ya kuanza kwa kasi tangu asajiliwe na mabingwa wa kihistoria katika klabu ya Yanga, straika Heritier Makambo, amekumbwa na ukame wa mabao.

Makambo ambaye alitua Yanga na kuteka vyombo vya habari, alianza kwa kasi kwa kutupia mabao kadhaa kwenye mechi za kirafiki.

Tangu kuanza msimu huu Makambo ameingia kambani mara mbili kwa kuzifunga Mtibwa na Coastal Union lakini katika mechi nyinginr hajabahatika kucheka na nyavu.

Kutokana na ukame huo mfupi, baadhi ya mashabiki wa Yanga wameanza kuhoji inakuwaje straika wao hatupii lakini wengine wakiamini ni suala la kumpa muda.

Kiungo Mshambuliaji, Ibrahim Ajibu ambaye aliwahi kuichezea Simba ndiye amekuwa gumzo hivi sasa kutokana na kuisaidia timu yake kupata alama tatu katika mechi takribani nne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic