October 16, 2018




Mambo si mazuri katika klabu ya Lipuli FC licha ya kwamba uongozi wake unajaribu kufanya jambo hilo ni siri kubwa.

Wachezaji hawajalipwa mishahara yao kwa miezi miwili sasa na wako wanaodai fedha zao za usajili.

Mmoja wa wachezaji wa Lipuli FC, ameiambia SALEHJEMBE kwamba hawana furaha na morali yao inashuka kutokana na kutolipwa.

“Hali si nzuri, uongozi umetupa ahadi nyingi lakini mambo si mazuri,” alisema.

Mchezaji mwingine amesema yeye na wenzake wamekuwa wakidai fedha zao za usajili bila ya mafanikio na wako ambao wanaona ikizidi, watarejea makwao.

“Unajua angalau basi upunguziwe kidogo, kaka watu tuna familia na tumekaa nazo mbali tukijua tupo kazini na ukipata kitu unatuma. Sasa uko mbali na nyumbani, unafanya kazi na hakuna unachopata. Wakati mwingine unajiona kama hauna akili,” alisema.

Juhudi za kuupata uongozi wa Lipuli FC zinaendelea. Awali, simu za viongozi wake zilikuwa hazipatikani na moja haikupokelewa.

TUTARUDI.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic