October 29, 2018


Ofisa habari wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba Haji Manara ameongezewa majukumu mengine ya kufanya mbali na kuwa ofisa atakuwa balozi wa kampuni kubwa inayoaminika kutoa ajira kwa vijana na kutoa sapoti kwenye sekta ya michezo.

Manara amesema kuwa kwake ni faraja kuweza kuongezewa majukumu, kwani ni heshima na fahari hasa kuwa balozi wa kampuni kubwa nchini.

"Nawashukuru Asas kwa kunipa heshima kubwa ya kuwa balozi wa bidhaa zenu na kampuni yenu kubwa kabisa nitatumia vipawa vyangu kuhakikisha nakuza taswira ya kampuni," alisema.

Manara amekuwa na furaha kubwa baada ya kuona amefanikiwa kumpapasa mpinzani wake Masau Bwire kwa kuwa alishindwa kumjibu kutokana na ushindani wa Ligi ulivyo, ameteuliwa kuwa balozi wa kampuni ya Asas pia ni Ofisa habari wa Simba hivyo majukumu kwake yameongezeka.

1 COMMENTS:

  1. Hakuogompa kumjibu Masawe Bwire ila alimuonea huruma maana alijuwa nini kitampata baada ya mechi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic