Imebainika kuwa ushindi waliopata jana Simba dhidi ya Ruvu Shooting wa mabao 5-0 ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Magufuli.
Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kabla ya mchezo aliwaambia wachezaji wacheze kwa ajili ya kutoa zawadi kwa Magufuli kwa kuwa aliwapa makavu siku walipofungwa akishuhudia mchezo wa ligi kuu msimu uliopita dhidi ya Kagera waliopoteza kwa bao 1-0 na leo ni siku yake ya kuzaliwa.
"Tumeyafanyia kazi kikamilifu hasa baada ya maelekezo ya Mheshimiwa kutaka tufanye vizuri katika mashindano ya klabu bingwa Afrika, tutatekeleza kwa vitendo maagizo yako na tunakatia kheri na fanaka ya kuzaliwa," alisema.
Rais Magufuli alisema kuwa Simba wamecheza mchezo mbovu hali ambayo iliwafanya waruhusu Kagera iwatoboe tundu, kama wataendelea kucheza hivyo hawataweza kuleta ushindani kwenye mashindano ya kimataifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment