October 30, 2018


Kocha wa timu ya Lipuli FC ya Iringa, Selemani Matola amesema kuwa atatumia uzoefu wa ligi kuwafunga wapinzani wake Yanga katika mchezo utakaochezwaleo saa 1:00 usiku, Uwanja wa Taifa.

Matola amesema kuwa hana mashaka na wachezaji wake kwa kuwa amewapa mbinu ambazo zitawasaidia kuweza kuibuka na ushindi.

"Tunakwenda kwenye mchezo tukiwa tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo, mpira hauna matokeo ya kukariri bali ni uwanjani ndiko kuliko na matokeo hivyo tutapambana kuhakikisha tunashinda.

"Mpira una njia zake na kanuni zake pia nimewaambia kuwa nami pia nilikuwa mchezaji nawajua vizuri wapinzani wangu uzoefu nilionao utasaidia kuweza kupata matokeo, vijana wana morali kuweza kupata matokeo," alisema.

Matola alikuwa mchezaji na nahodha wa Simba kabla ya kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini ana imani kwamba uzoefu wake utamsaidia leo kuweza kuibuka na ushindi kutokana na kuzijua mbinu za wapinzani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic