October 30, 2018



Mshambuliaji wa timu ya Lipuli FC, Maalim Busungu ameibuka na kusema kuwa hajapotea yupo kwa sababu kuna mambo hayajakamilika ndani ya uongozi ndio maana amejiweka kando kwa muda.

Uongozi wa Lipuli ulisema kuwa Busungu alitoweka bila kuaga na kuweza kutojiunga na timu wakati walipokuwa wakijiandaa dhidi ya Mbao FC, mpaka sasa hajajulikana alipo kutokana na kutotoa taarifa kwa kuwa ni mtukutu.

"Nipo salama kwa kuwa niliamua kujiweka kando kutokana na kutokamilishiwa malipo yangu ya kimkataba kwa muda mrefu, nimetulia Dodoma kwa sasa sijaenda kambini mpaka sasa kwa sababu nawadai.

"Sijakaa kikao na uongozi mpaka sasa, nina mpango wa kuachana na mpira kwa kuwa nahitaji amani, nitafanya biashara zangu ili kuweza kuendelea na maisha," alisema.

Busungu alisajiliwa Lipuli msimu uliopita akitokea timu ya Yanga amekuwa na mgogoro na timu kutokana na kile alichodai ni kutolipwa maslahi yake huku uongozi ukisema kuwa yeye ni mkorofi ndani ya timu, hatakuepo leo katika kikosi kitakachoivaa Yanga uwanja wa Taifa.

1 COMMENTS:

  1. Sio maalim busungu ni malimi busungi fanya homework yako vizuri!! usituandikie upuuzi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic