October 4, 2018


Licha ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Ruvu Shooting, uongozi wa Mbao ya mkoani Mwanza umeibuka na kusema kuwa wana waheshimu Yanga kama timu kubwa lakini siku ya Jumapili watawasamehe tu kwani watatengeneza matokeo ya kuwafurahisha Simba.

Mbao ambao msimu huu wapo vizuri katika ligi kuu kwani katika michezo nane walicheza wameshinda minne na kutoka sare miwili na kufungwa miwili wakiwa na pointi 14 wakishika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu.

Kwa mujibu wa Spoti Xtra Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njashi alisema ; “Sisi kama Mbao naweza kusema msimu huu tumejipanga haswa kwani ukiangalia msimu uliopita na msimu huu ni tofauti sio kama tumeridhika na pointi hizi hapa tunaendelea kupambana lakini tunajua kuwa ligi msimu huu ni ngumu.”

5 COMMENTS:

  1. Mbao waliocheza michezo nane nakushinda minne suluhu mbili kupoteza mbili wakiwa na pts 14 anaonekana kuanza vizuri,lakini simba aliyecheza mechi 6 akashinda mbili suluhu tatu na kupoteza moja akiwa amekusanya pts 9 bado na viporo vyake viwili wanamponda eti simba kaanza vibaya.amakweli ukikichukia kitu hata kiwe vp lazima utakiponda tu.ndiomana kuna kale kamsemo wanasema AKIPENDA CHONGO HUITA KENGEZA.yanga bado sana kwa mpira mnaocheza Mbao watawafanya hakuna ngoja muone shoo jumapili.

    ReplyDelete
  2. Haah kwa Mchina, msitarajie kupata ushindi nyinyi Mbao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kijana Funga kinywa chako mbao wametoka kupigwa juzi hivyo ni ngumu sana kwa yanga kupata points 3 kirahisi,ugumu wa game uko hivyo yani haijalishi wapi kama kufungwa ni kufungwa tu.usipende kucheza mpira kwenye media na social networks utajipa stress ndugu yangu,angalia alliance wamemfunga kmc na inajulikana wazi kmc ni bora kuliko alliance but kilichofanyika ni pressure ya kupoteza ndio iliwapa ushindi alliance na ndivyo itakavykua kwa yanga na Mbao,Mbao wana pressure kubwa sana ya ushindi ndicho kitachoipa ugumu yanga,mkijitahidi sana labda sare.

      Delete
  3. siku ya jumapili mtoto hatumwi sokoni .mbao wanachezea kichapo mapema. tusubiri jumapili

    ReplyDelete
  4. Malengo ya mbao ni kuwafurahisha simba?,mbona waliwafunga !!!. Timu hii inaonyesha ni jinsi gani hawana malengo, inastahili kushuka daraja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic