October 4, 2018


Mkongwe na Kocha wa zamani wa klabu ya Simba, King Kibadeni, amesifia mbinu ambazo alizitumia Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera katika mechi iliyowakutanisha watani hao wa jadi Septemba 30.

Kibadeni ameeleza kuwa mbinu na mfumo alioutumia Zahera kweli alifanikiwa kwa kwenda suluhu tasa na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Mkongwe huyo ambaye aliwahi kufunga mabao matatu pekee 'Hat Trick' katika mechi iliyokutanisha timu hizo miaka ya nyuma, amempongeza Zahera kwa lengo lake kufanikiwa.

Licha ya kipa Beno Kakolanya kufanikiwa kuokoa kwa jitihada zote mashabulizi kutoka kwa straika hatari wa Simba, Kibadeni anaamini Zahera alikuwa na mchango wake.

8 COMMENTS:

  1. Kama kweli King kibadeni amekoshwa na jinsi Yanga ilivyocheza zidi ya Simba Jumapili,kama kweli itakuwa hakulishiwa maneno basi atakuwa uzee unaanza kumletea madhara. Inafahamika yakwamba Yanga inatumia nguvu kubwa kupitia vyombo vya habari kujaribu kuwaaminisha watu kuwa katika mechi ile ya Jumapili zidi ya Simba hawakuwa wamezidiwa bali ndio walipanga kucheza vile? Mjinga gani anejua mpira atakaekubali kudanganjwa wakati mchezo wa mpira unachezwa hadharani na takwimu zake kila kitu. Kinachokera zaidi Yanga kashindwa kucheza mpira uwanjani na badala yake wameamua kwenda kuucheza kwenye vyombo vya habari wakipiga chenga na kuwazidi hata Simba kipasentage na mashuti ya kulenga goli ni ujinga kabisa. Kusema kweli kocha Zahera aliingia uwanjani na mikakati na Mbinu za kumchinja mnyama na alijiaminisha kuwa yupo tayari kwa Simba lakini Simba walikuja kivingine na kupindua meza na kuifanya Yanga kuonekana nyanya. Kila kitu huwa na bahati pia la sivyo Yanga walikwisha ingia kwenye himaya ya Mnyama walibakia kuliwa tu hongera kwa benchi la ufundi la Simba kwani mechi zote alizoshinda Yanga watu ilibidi wajiulize walishindaje kutoka kwa kikosi dhaifu kama kile zidi ya Simba. Mfano Simba ingekuwa ndio Yanga katika mechi ile watu na waadishi wapambe wa Yanga wangesemaje? Au kibadeni angejisikia vizuri kumsifia kocha wake wa Simba?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Basi simba mngeshinda sasa kelele za nini unatumia nguvu kubwaa kupinga

      Delete
    2. Kwa hiyo Simba ilishinda? Kibadeni ni kocha anajua anachokisema na mpira ameucheza.

      Delete
    3. This comment has been removed by the author.

      Delete
  2. Kupaki basi ni mbinu dhaifu unapokuwa dhaifu zaidi ya mpinzani wako.Mourinho anapondwa kila siku kwa mbinu hiyo ya kutoamini wachezaji wake.Wengi wa wachambuzi wanaiita Anti football.Kibadeni amesema mbinu hiyo ilimsaidia kocha wa Yanga hakusema amekoshwa. Ndio maana haitatokea Klopp au Pep Guardiola amepaki basi.

    ReplyDelete
  3. Tatizo Simba hawatakagi kuambiwa ukweli wakakubali, Mpira na mbinu wanazotumia Simba ni ile alikuwa anatumia Arnen Wenga, kumiliki mpira na kufunga magoli kwa staili ile ile, Mwisho wa siku matokeo yanasuasuaAnliochezandanda, Angalia mpirocheza nwaliongoza kwa kila kitu, Angalia pia mechi yao na Mbao Waliongoza 76% kwa 24%, Team inapochezainapa na simba isipofungSimba wanakuwa katika hali ngumu, lakini wakifunguka wanapigwa mengi

    ReplyDelete
  4. King Kibadeni,wewe ni bonge LA kocha ulie salia Tz.japo kuwa inachembechembe za unyamanyama(,usimbasimba) ndani yako,lakini umeutazama Mpira ule kiufundi zaidi,kitaaluma zaidi.
    Kupaki bus ni ujanja ns mbinu ya mchezo.ni dehrmu ya Moira Wa wajanja na wenye skili.ni sawa na kipa kulals na Moira akiuza muda au kuwapumzisha wavhezaji wake,kutoa Moira inje mars Kwa mpira inje ili kuja muda.kumzongga zonga zonga refa yaani kutengeneza malalamiko Kwa refa ilii muda uende.haya ni mambo ambayo makocha mafundi hutengeneza baada ya kuisoma timu pinzanni.
    Huo ndio msingi uliompelekea King Kibadeni kutamka hayo.yaani ile taaluma yake kimpira.sio ushabiki.
    Mbona inajulikana Simba anakikosi bora kuliko Yanga.hii inajulikana hats na chekechea.na Kwa kutambua ubora huo Wa Yanga Zahera bingwa Wa mbinu na ubora Wa fikra za kimpira aliagiza wachezaji Wa Yanga wamwachie mnyama acheze yeye Moira..maana shida ya Yanga walikuwa hwana presha ya kutafauta goli Bali wao walittafuta ushindi Wa ugeni ZAHERA alifanikiwa.Sasa msikilize kocha Wa simba anavyolia ,eti oho ohoh tangu Sasa nitawnitaweka straika akina salamba waanze.anakumbuka blanketi wakati kumekucha!!!Kwa vyovyote Moira ule Yanga waliibuka washindi na waliwabana simba kiufundi,mbinu na akili.huo ndio Moira Wa Leo.poleni.endeleeni kucheza Moira Wa Hana wakufurahisha mashabiki kisha mnatoka bila matokeo.Moira na mbinu iletayo matokeo unayoyataka.

    ReplyDelete
  5. Tanzania ndio nchi pekee ambayo uongo unanguvu. Kuliko ukweli.naamini mashabki wa yanga ni vipofu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic