October 4, 2018


Kufuatia uongozi wa klabu ya Yanga jana kueleza hadharani kuwa umetuma baria kwenda Shirikisho la Soka nchini (TFF). uongozi wa Simba nao umeibuka na kuliibua suala la mchezaji Andrew Vincent kumtishia kichwa Mohammed Hussein.

Yanga waliitisha kikao na waandishi wa habari jana kunako makao makuu ya klabu hiyo na kueleza kuwa walisitishwa na kitendo cha kiungo wa Simba, James Kotei kumpiga beki wao Gadiel Michael.

Baada ya tukio hilo, Yanga waliamua kukaa chini na kufikia maamuzi ya kupeleka malalamiko TFF ili Kotei aweze kuadhibiwa kutokana na kucheza mchezo usio wa kiungwana.

Licha ya Yanga kufanya maamuzi hayo, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameibuka na kulipua bomu kwa kueleza kuwa hata wao waliona alichofanyiwa mchezaji wao lakini waliamua kukaa kimya.

Manara ameeleza kuwa katika mechi hiyo, beki wao Dante alimtishia kumpiga kichwa Hussein lakini waliamua tu kukaa kimya.

Ofisa huyo mwenye maneno mengi amesema ifikie hatua wachezaji wote si Simba wala Yanga waache kuonesha vitendo ambavyo si vya kiungwana ili kutokuharibu taswira ya mchezo wa soka.

1 COMMENTS:

  1. Hizo ni mbwembwe za fitina za MANALA kutishia hilo na kupooza makali ya shitaka la Kotei.Yeye akitaka naye speleke hill shitska L's Vincent hiko TFF watalichunguza nalo na hatua zitachukuliwa.Yanga msikae kimya mkomae juu ya Kotei hadi kielewee.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic