October 10, 2018


Mlinda Mlango wa klabu ya Yanga, Beno Kakolanya, pengine inawezekana akawa amezua hofu kubwa ndani ya timu yake kufuatia kuumia katika mchezo wa mwisho walipocheza na Mbao FC.

Mpaka kufikia jana ilikuwa haijajulikana kama Kakolanya atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaosafiri kuelekea Cape Verde kwa ajili ya kibarua cha mchezo wa kuwania kufuzu AFCON.

Kakolanya aliumia walipocheza na Mbao na kuepelekea hofu kwa mashabiki wengi na wanachama wa timu hiyo kutokana na umahiri wake wa kudaka mipira langoni.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinasema hali ya kiafya kwa mchezaji huyo inaendelea vema na haitaweza kuchukua muda mrefu kwake kuwa fiti.

Tayari kikosi cha Stars kimeshaondoka kuelekea Cape Verde kukipiga na wenyeji wao katika mchezo wa kundi L wakiwa na kumbukumbu ya kwenda suluhu tasa na Uganda kwenye mechi ya mwisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic