October 10, 2018


Baada ya kuzuka tetesi jana juu ya Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu ya KRC Genk huko Ulaya, wakala wa mchezaji huyo, Jamali Kisongo, ameibuka na kukanusha habari hizo.

Iliripotiwa kuwa Samatta ameanza kuwindwa na timu kadhaa zinazoshiriki Ligi Kuu England ikiwemo Everton, Brighton, West Ham na Aston Villa.

Kisongo amesema kuwa hizo ni tetesi tu ambazo zimezushwa na hazina ukweli wowote juu ya mchezaji wake kuelekea huko.

Aidha, Kisongo amesema hakuna haja ya kuzidi kuzisambaza zaidi kwani zinaweza zikamuathiri Samatta ambaye nguvu zake zote hivi sasa ziko ndani ya klabu yake.

Mshambuliaji huyo tegemo ndani ya timu hiyo amesafiri na kikosi cha Stars usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo dhidi ya Cape Verde utakaopigwa Oktoba 12 2018.

3 COMMENTS:

  1. Sasa cha kukanusha hapo kitu gani? Wakati kuna habari za uhakika kutoka club tajwa za uiengereza kuwa zina nia ya kumsajili Samata. Wakuwaambia waachane na habari hizo ni wa waengereza waliosambaza hizo habari lakini sio watanzania watu wengine vipi lakini?

    ReplyDelete
  2. Kwenye website ya Everton habari hiyo ipo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic