NAMNA ULINZI ULIVYO KUFURU NYUMBANI KWA MO
Gumzo kubwa kwa sasa ni tukio la kutekwa kwa bilionea mkubwa Tanzania, Mohammed Dewji ‘Mo’ ambapo utekaji huo umesababisha ulinzi mkubwa kuwekwa nyumbani kwake, Masaki jijini Dar es Salaam, Risasi limejionea.
Mo alitekwa juzi, Alhamisi ya Oktoba 11, 2018 alfajiri na wazungu wasiojulikana akiwa katika eneo la Hoteli ya Colloseum iliyopo Oysterbay jijini Dar ambapo alifika kwa ajili ya kufanya mazoezi.
Baada ya tukio hilo lililotikisa nchi, waandishi wetu walifika nyumbani kwa tajiri huyo ili kuzungumza na ndugu, jamaa na marafiki akiwemo mkewe lakini walikutana na mazingira magumu kufuatia walinzi wa Kampuni ya KK Security kutanda kila kona.
“Kama siyo ndugu huruhusiwi kupita hapa, mnajua hali siyo shwari kwa hiyo kama unajijua huhusiki eneo hilo, chapa lapa,” alichimba mkwara mmoja kati ya askari hao.
Wakati waandishi hao wakiangalia ustaarabu wa kuondoka eneo hilo ili kuepusha shari, mmoja wa walinzi alisikika akimwambia mwenzake kuwa, inabidi wawasiliane na ofisi kuu ya kampuni yao ili kuimarisha zaidi ulinzi kutokana kile kilichotokea.
Kwa mujibu Risasi, jirani wa Mo aliyejitambulisha kwa jina la Fred, alisema tangu bilionea huyo kijana atekwe, nyumbani hapo ulinzi umeongezeka.
“Leo walinzi wameongezwa, tena wenye silaha na ndiyo maana huoni mtu akirandaranda pale, kama siyo ndugu kuingia mle ndani sasa hivi ni shughuli pevu, utakaguliwa mpaka basi,” alisema jirani huyo na kuongeza.
“Unajua waliomteka hawajajulikana ni akina nani na walikuwa na nia gani, kwa hiyo hata mkewe na ndugu zake wengine wamewekewa ulinzi mkali maana isije ikatokea na wao wakatekwa.”
Jinsi alivyotekwa Taarifa zilieleza kuwa, Mo ambaye ni mwekezaji wa Klabu ya Soka ya Simba ya jijini Dar, alitekwa alipokuwa akiingia ‘gym’ katika Hoteli ya Colloseum na kwamba waliomteka walifika mapema kisha alipofika walimchukua na kupiga risasi juu na kuondoka naye.
“Mara tu baada ya kushuka kwenye gari lake alilofika nalo aina ya Range Rover lenye rangi nyeusi ndipo wakatokea watu hao wasiojulikana kisha wakamchukua, wakapiga risasi juu na kuondoka naye kuelekea kusikojulikana,” alisema mmoja wa mashuhuda bila kutaja jina.
“Unajua waliomteka hawajajulikana ni akina nani na walikuwa na nia gani, kwa hiyo hata mkewe na ndugu zake wengine wamewekewa ulinzi mkali maana isije ikatokea na wao wakatekwa.” Jinsi alivyotekwa Taarifa zilieleza kuwa, Mo ambaye ni mwekezaji wa Klabu ya Soka ya Simba ya jijini Dar, alitekwa alipokuwa akiingia ‘gym’ katika Hoteli ya Colloseum na kwamba waliomteka walifika mapema kisha alipofika walimchukua na kupiga risasi juu na kuondoka naye.
“Mara tu baada ya kushuka kwenye gari lake alilofika nalo aina ya Range Rover lenye rangi nyeusi ndipo wakatokea watu hao wasiojulikana kisha wakamchukua, wakapiga risasi juu na kuondoka naye kuelekea kusikojulikana,” alisema mmoja wa mashuhuda bila kutaja jina.
0 COMMENTS:
Post a Comment