October 14, 2018


Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Kangi Lugola, jana wataka wafanyabiashara wakubwa na watu maarufu kuwa makini na suala la ulinzi wao binafsi.

Kwa mujibu wa Spoti Xtra, Lugola alisema hayo kutokana na tukio la kutekwa kwa Mfanyabishara kijana na bilionea, Mohammed Dewji 'Mo' akieleza kuwa ni muhimu kwa usalama wao. 

“Suala la kujihakikishia usalama binafsi ni jambo muhimu sana kwa hawa watu,”alisema Kangi ambaye ni Mbunge wa Mwibala tangu mwaka 2010. 

Mashabiki hususani wa Simba wamekuwa wakijiuliza kuhusiana na kama MO alikuwa na ulinzi binafsi au la ingawa habari za awali zinadai kwamba alivyotekwa hakuwa na mlinzi alikuwa mwenyewe.

Kauli hii ya Lugola ina maanisha kuwa matajiri wengine wakubwa hapa nchini akiwemo Yusuf Manji ambaye amewahi kuwa mfadhili na kiongozi wa Yanga wanatakiwa kujiwekea ulinzi wa kutosha ili kuepuka kukumbwa na hali kama hii ya Mo.

1 COMMENTS:

  1. Hatari sana, Mungu atunusuru lakini baadhi ya kauli zinapaswa kuchungwa zisemwapo maana badala ya tahadhari inaweza kuonekana ni kitisho na hawako salama tena wenye ukwasi. Nadhani ni vema vyombo vya usalama vikawajibika kadri ya uwezo wao kudhibiti hali nasi raia ni vema kuwa na ushirikiano na vyombo vya usalama pasina kutiliana mashaka kwa usalama wetu sote.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic