Kiungo wa timu ya Yanga, aliyejiliwa msimu huu akitokea timu ya Mtibwa Sugar, Mohamed IOssa 'Banka' atauwahi mchezo wao dhidi ya Simba ambao utachezwa mwakani Februari 16 baada ya kuadhibiwa na Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni ya Kanda Tano Afrika (RADO).
RADO imetoa hukumu ya kumfungia 'Banka' kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya Bangi, baada ya kumkuta na hatia na yeye mwenyewe kukiri kwa kutoa maelezo ya maandishi baada ya kutakiwa kukubali ama kukataa kosa utetezi uliowakilishwa Agosti Mosi mwaka huu.
Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema kuwa wakati wote huo Banka hataruhusiwa kufanya chochote kinachohusiana na michezo ikiwa ni kufanya mazoezi hadharani au kuonekana akishiriki shughuli za mpira wa miguu.
" Baada ya uchunguzi wa maabara na utetezi toka kwa mchezaji huyo, Kamati imemkuta na hatia na imemfungia kwa kipindi cha miezi 14 kuanzia Desemba 9,2017 na adhabu inatarajiwa kumalizika Februari 8,2019," alisema.
Mnamo Desemba 9,2017 Banka akiwa Machakos nchini Kenya walipokuwa kwenye michuano ya CECAFA Chalenji, akiwa na timu ya Zanzibar iliyoshika nafasi ya pili, alichukuliwa vipimo vya mkojo vilisafirishwa kwenda maabara ya WADA iliyopo Doha, Qatar kwa uchunguzi zaidi na majibu kurudi yakiwa na tuhuma hizo zinazomkabili.
0 COMMENTS:
Post a Comment