October 31, 2018


Uongozi wa timu ya Simba umesema kuwa wapo tofauti katika mfumo wa kucheza hali inayofanya waweze kupata matokeo na kuwaachia dongo wapinzani wao Yanga kimtindo kwa kudai wanacheza kwa kujilinda.

Ikumbukwe kuwa mpaka sasa Yanga hawajapoteza mchezo hata mmoja kati ya tisa waliyocheza baada ya kushinda michezo 8 na kutoa sare dhidi ya Simba, ambapo kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alisema kama utashindwa kufunga basi zuia kufungwa.

Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema mfumo wa Simba wa muda wote ni kupata matokeo na kucheza soka la burudani.

"Falsafa ya Simba miaka yote ni kucheza na kupata matokeo chanya, tuna wachezaji makini kama Claytous Chama, Shomari Kapombe na wengine wote wanafanya maajabu ambayo yatakufanya usichoke kuangalia mchezo wa Simba.

" Hatuna faslasa ya piga mbele, haibutuibutui mipira wala kucheza soka la kujilinda bali inashambulia na kukuburudisha hali ambayo haichoshi kuitazama hii yote inatokana na mfumo wa Kocha Patrick Aussems, soka la Simba kwa sasa limepiga hatua kubwa," alisema.

Katika michezo minne mfululizo waliyocheza Simba dhidi ya African Lyon, Stand United, Alliance na Ruvu Shooting wamefanikiwa kukusanya jumla ya mabao 15 na pointi 12 yote wamecheza Uwanja wa Taifa .

11 COMMENTS:

  1. Ndio maana wakafungwa na Mbao Fc kwa mchezo huo wa kuburudisha!

    ReplyDelete
  2. Yanga ni point 3 bila kujal idadi ya magoli mengi bingwa huamuliwa kwa points nyingi hizo chenga twawala hazna nafasi jangwan tunataka arudi mwali mahali lake jangwan
    Mipasho peleka mwambao Mpira unachezwa hazaran
    Chumba namba 3 imewakubali huku mnapiga kelele eti timu nzri

    ReplyDelete
  3. Yanga mnakazi ngunu mnafurahia kucheza dar tu mzunguko2 mtaisoma namba wakati timu zinapapana ilizcshuke daraja ijuma simba itakua tanga na jkt Tanzania kazi ni kwenu

    ReplyDelete
  4. Ha ha ha ha kazi wanayo ngoja wamalizie EDA yao waanze kutoka nnje wataerewa tu.

    ReplyDelete
  5. Ha ha ha ha kazi wanayo ngoja wamalizie EDA yao waanze kutoka nnje wataerewa tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mm nawashangaa washabiki wa mkia angalien timu yenu kwan sisi kupata goli moja inawauma nn wakat hilo goli moja Kwa ngurue watoto 10 sasa unashaa nn achen umbea fanyeni yenu

      Delete
  6. Kama unacheza Dar unapata goli moja...hivi huko mkoani tutapata hill moja pia..Labda safe na kufungwa

    ReplyDelete
  7. Kama unacheza Dar unapata goli moja...hivi huko mkoani tutapata hill moja pia..Labda safe na kufungwa

    ReplyDelete
  8. Tangu mpigwe cha nguruwe huko Mwanza ndio kila kitu imekuwa mikoani, Msimu uliopita mlipigwa na Kagera 2 -1 wakati Yanga alimpiga za kutosha kwenye uwanja wa Bukoba. Lipuli waliwapiga pale iringa wakati Yanga alimtandika pale pale mbili kavu! Acheni zenu MIKIA!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic