October 9, 2018


Straika Mganda wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi, ameibuka na kueleza kuwa kwa sasa ukurasa wake umefunguka rasmi baada ya kutupia bao moja dhidi ya African Lyon.

Okwi alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza Jumamosi ya wiki jana katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam huku timu hiyo ikishinda kwa mabao 2-1.

Straika ameeleza kuwa bao hilo linakuwa linampa nguvu ya kuendelea kupambana zaidi ili kufunga mengine baada ya kucheza mechi takribani 6 bila kugusa nyavu za wapinzani.

Hata hivyo Okwi ameeleza kutojutia kukosa mabao mengi kwa nafasi alizozitengeneza jambo ambalo analichukulia kama sehemu ya matokeo ya mpira wa miguu.

Katika mechi hiyo dhidi ya Lyon, bao jingine la Simba liliwekwa kimiani na Shiza Kichuya ambaye pia alikuwa anafunga kwa mara ya kwanza msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic